Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire akizungumza na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Jumatano Septemba 27,2023
Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire akizungumza na waandishi wa habari Mjini Shinyanga leo Jumatano Septemba 27,2023
Na mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Timu ya mpira wa Miguu ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)Tanzania imethibisha rasmi kutumia uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kama uwanja wake wa nyumbani katika michezo yote ya Ligu Kuu ya NBC -Tanzania hadi pale uwanja wao wa Meja Jenerali Isamuyo uliopo Mbweni Dar es salaam utakapokamilika baada ya matengenezo makubwa yanayoendelea kufanyika.
Hayo yameelezwa na Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya JKT Tanzania, Masau Bwire katika Mkutano wake na vyombo vya habari Mjini Shinyanga leo Septemba 27,2023.
Amesema wameuchagua uwanja wa CCM Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani kwani wanataka maeneo yote nchini yanapata fursa hivyo furaha ya JKT Tanzania ni kuona wakazi wa Shinyanga wanapata furaha ya Soka hivyo kuwaomba wakazi wa Mkoa huo kuipa ushirikiano timu hiyo.
"Tutatumia uwanja huu hadi uwanja wetu utakapokamilika matengenezo..Uwanja wa CCM Kambarage umepitishwa na TFF kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya mechi za ligi kuu ya NBC. Na tutaanza kuutumia uwanja huu katika Mchezo wetu na Kagera Sugar utakaofanyika Ijumaa hii Septemba 29,2023 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme",amesema Bwire.
"Tunaomba wakazi wa Shinyanga waichukue na kuipokea JKT Tanzania kama timu ya nyumbani na kuipa ushirikianao wote katika kuendelea kutumia uwanja wa CCM Kambarage", ameongeza Bwire.
Mechi ya Kagera Sugar na JKT Tanzania inayotarajiwa kufanyika Septemba 29,2023 utakuwa na viingilio rafiki ili kila mmoja kushiriki katika mechi hiyo na shinyanga imekuwa na ukame wa muda mrefu wa kukosa mechi za ligi kuu.
"Double K ni kichapo cha kizalendo kiheshimike kwa kuwa kila timu itakayofika hapa lazima ipate kichapo. Mechi ya Ijumaa na Kagera Sugar ni kichapo cha kizalendo, Kagera Sugar tutaipa Double K kwani tuna kikosi bora na makini na wachezaji wenye vipawa zaidi",amesema.
"Tumepanga kiingilio ni Tshs 2000/= kwa mzunguko na Jukwaa kuu ni Tshs 3000/= kwa maana ya jukwaa kuu. Pia Mfumo wa N Card utatumika ili kusaidia kutoa huduma kwa mashibiki kukata tiketi zao
"Tunatumia N Card ili kuepusha msongamano na malalamiko na tumewasiliana na mamlaka husika wa kutekeleza jukumu hilo kutoka Dar es salaam na ofisi ya TTCL na utaratibu wa kuuza tiketi utafanyika katika vituo vya Soko Kuu, Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na ofisi za TTCL Shinyanga na siku ya mechi mageti katika uwanja wa CCM Kambarage yatafunguliwa kuanzia saa 4:00 asubuhi.
"Tungependa mashabiki wetu waje na sura ya JKT siku ya mechi kwa kuvaa jezi zenye ubora ambazo zinapatikana kwa Tshs 35,000/= na kofia kwa Tshs 10,000/=",ameeleza.
0 comments:
Post a Comment