Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri,akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo kuhusu mfumo wa Anwani za Makazi kwa Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.
Mratibu wa Anwani za Makazi Kitaifa kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Jampyon Mbugi,akitoa maelezo kuhusu Mafunzo ya kujenga uwezo wa Mfumo wa Anwani za Makazi Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri (hayupo pichani) wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amewataka Maofisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuwa anuani za makazi ni hitaji la msingi kwasasa kutokana na kukua kwa teknolojia nchini.
Shekimweri ameyasema hayo leo Septemba 14,2023 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kujenga uwezo Maafisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi.
“Kwa sasa hivi ni rahisi kuita gari la kukodi (Uber) ukaonesha eneo unapokwenda na huduma hiyo ikakufikia, hivyo unaweza kuita huduma ukiwa nyumbani kwako,”amesema Bw.Shekimweri
Amesema kuwa taarifa zinaonesha kwamba uwepo mfumo wa anwani za makazi nchini tayari umeleta mafanikio makubwa katika utendaji kazi wa serikali ikiwamo ufuatiliaji wa kodi za serikali.
“Zoezi hili ni lazima likatekelezwe kutokana na Jiji linakua kwa kasi, makazi yanaongezeka, mitaa inaongezeka hakuna namna zaidi ya kuziingiza taarifa hizi kwenye mifumo yetu, zoezi hili ili lifanyike kwa mafanikio ni lazima liwe shirikishi hasa madiwani hivyo kwenye mpango kazi muone umuhimu wa kuwashirikisha,”amesema
Hata hivyo ametoa wito kupitia vikao vya kisheria ikiwamo Mabaraza ya madiwani kupewa muda wa kuwasilisha elimu ya suala hilo na wajibu wao wa kuhamasisha wananchi kujisajili na mfumo wa anwani za makazi.
Kwa upande wake Mratibu wa Anwani za Makazi Kitaifa kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Jampyon Mbugi, amesema hadi sasa Jiji la Dodoma limekusanya taarifa na kutoa anuani za makazi 245,000 kati ya hizo 163,000 ni za majengo na 81,277 ni viwanja vitupu.
“Wananchi 299,330 ndio waliosajiliwa kwenye mfumo wa anwani za makazi, idadi hii haiakisi uhalisia wa takwimu za idadi watu waliopo ndani ya Jiji la Dodoma inayokadiriwa kuwa zaidi ya 765,000,”alisema.
Aidha amesema kuwa zaidi ya wananchi 465,849 hawajasajiliwa kwenye mfumo huo na hivyo serikali imeamua kuongeza msukumo wa suala hilo hususan kwa kutumia Wenyeviti, Watendaji wa Kata na Mitaa.
''Dhamira ya Wizara ni kuhakikisha Dodoma inakuwa ya mfano na kuwa chachu kwa halmashauri zingine kuja kujifunza namna ya kufanikisha utekelezaji wa mfumo huo.''amesma Mhandisi Mbugi
0 comments:
Post a Comment