Friday, 29 September 2023

USAILI “INTERVIEW” SEKRETARIETI YA AJIRA DODOMA KIZUNGUMKUTI ‘JINSI MARIUM ABDUL” ALIVYONYIMWA HAKI YAKE YA MSINGI YA KUFANYA USAILI,BAADHI YA MAOFISA KUJIITA MIUNGU WATU MFANO:ALLY MTUMISHI SEKRETARIETI YA AJIRA

...

 


Na mwandishi Maswayetu blog;



Baada ya Serikali ya Jamhuri ya MUUNGANO kuhakikisha kwamba nafasi za kazi zote Tanzania zinatolewa kwa usawa na uwazi kwa vijana wote wanaopambana kutafuta kazi Serikalini,kumekuwa na changamoto nyingi katika usaili huo ambao wafanyakazi wake wamegeuka Miungu Mtu.

Hadithi ya Marium,inaanza Tangu alivyomaliza Chuo mwaka 2016,Chuo kikuu cha kilimo Sua shahada ya sayansi ya Kilimo. Alikuwa na mategemeo makubwa sana ya kuajiriwa kutokana na mifumo ya aliekuwa Rais wa awamu yan ne Dkt.Kikwete,lakini ndoto zake zilizimika ghafla baada ya mabadiliko ya uongozi yaliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambao ulimpa Nafasi ya kuongoza nchi aliekuwa Rais wa Awamu ya 5 Dkt.Magufuli.

Ajira zilisimamishwa ghafla na kumfanya Marium ambae tangu anasoma wakati huo akili yake ilikuwa kuajiriwa serikalini kupoteza uelekeo wa Maisha.Alikaa mtaani kuanzia mwaka 2016 mpaka 2022 ambapo ajira zilianza kutangazwa upya tena kupitia sekretarieti ya ajira iliyopewa mamlaka hayo.

Marium aliomba kazi zilipotangazwa na alifanikiwa kuitwa kwenye usaili Mjini Dodoma ,ambapo katika nafasi 5 zilizotangazwa waliitwa vijana Zaidi ya 3879 kugombania nafasi hizo(hii ilitokana na wingi wa wahitimu waliokosa kuajiriwa kuanzia mwaka 2016 mpaka 2022).

Tangazo hilo la usaili lilimkuta Marium akiwa mjini Moshi,hivyo kumfanya ajikusanye nauli na kufunga safari kutoka Mosho hadi Dodoma kwa ajili ya kuhakikisha anapambana kuweza kuajiriwa. Alifika Dodoma akiwa kamili na vyeti vyake,siku ilipofika aliwasili mapema yalipo majengo ya chou kikuu cha Dodoma (udom) kwa ajili ya kufanya usaili huo.

Afisa wa Ajira aitwae Ally aliwasili akiwa yeye ndio incharge wa zoezi hilo siku hiyo,alitangaza waliofika kwa ajili ya usaili shahada ya kilimo waendeo chumba namba 3,alianza kukagua vyeti kama ni original, Marium alikuwa nav yeti origina vyote ilipofika katika zoezi la vitambulisho,kitambulisho cha Marium kilikuwa kwenye simu yake (soft copy) alikataliwa na kuwekwa pembeni.Marium alishtuka sana ,akauliza anaweza kwenda kufatilia barua kwa mtendaji? Akaambiwa subiri,kumbuka ilikuwa saa 1 asubuhi,lakini walikalikshwa mpaka saa 3 asubuhi,ndipo taarifa ilitoka kwamba wanatakiwa kurudi nyumbani kwani hawana sifa ya kufanya mtihani,huku wenzao wakianza mtihani wa dk 40 muda huo.

Marium alilia sana,kumbuka kapoteza mud ana pesa ,pia alichokifata kakikosa, Alimfata Ally na kumsihi amruhusu akafanye mtihani,lakini Ally alijinasibu kwamba ana “MIAKA 10 KAZINI YA UZOEFU” hivyo hizo janja janja anazijua, na KUSEMA KWAMBA “Yeye akitamka ndio mwanzo na mwisho” hivyo waondoke tu.

Marium alirudi nyumbani na kukosa haki yake ya msingi,Lakini Mungu si Amina wala Juma,zilizotoka nafasi nyingine Marium aliomba na kufanikiwa kufika Dodoma kwa ajili ya usaili,alifanya mtihani ,akafaulu kwenda oral akiwa na maksi za juu kabisa, na sasa ameajiriwa Baraza la mitihani kama Afisa wa baraza(NECTA).

 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger