Thursday 21 September 2023

KIMBUNGA CHAUA WATU 10 CHINA

...

Watu kumi wamefariki dunia wakati kimbunga kikali kikipiga katika miji miwili katika jimbo la Jiangsu mashariki mwa China.

Hilo ni tukio la hivi karibuni la hali mbaya ya hewa kuikumba nchi hiyo, ambayo katika miezi michache iliyopita imekuwa ikikumbwa na mafuriko makubwa pamoja na mawimbi ya joto kali.

Watu wengine wannewamejeruhiwa vibaya kutokana na kimbunga kikali kilichopiga mji wa Suqian katika jimbo la Jiangsu siku ya Jumanne, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha serikali CCTV. Mkoa huo uko katika pwani ya mashariki ya China.

Zaidi ya watu 400 wamehamishwa na zaidi ya nyumba 130 zimeharibiwa katika mji huo, CCTV iliripoti.

Kwa upande mwingine, kimbunga chenye nguvu zaidi kilisababisha vifo vya watu watano na wanne wakiwa na majeraha madogo Jumanne usiku huko Yancheng - ambayo iko kusini mashariki mwa mji wa Suqian na kaskazini mwa mji mkubwa wa China, Shanghai - CCTV imesema, na kuongeza kuwa watu 129 wamehamishwa.

Tornadoes sio kawaida katikati ya Septemba huko Jiangsu, lakini kimbunga adimu kimetokea kutokana na joto la juu la hivi karibuni ambalo limeleta hali ya hewa kali, vyombo vya habari vya serikali Beijing Youth Daily iliripoti, ikinukuu wataalam wa hali ya hewa.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger