Friday 22 September 2023

WADAU WAVUTIWA NA BANDA LA GST KATIKA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI MKOANI GEITA

...




Wadau wa sekta ya Madini waona umuhimu wa kutumia taarifa za GST

Wadau mbalimbali wameeleza kuvutiwa na kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania kinachopatikana katika Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) lililopo kwenye maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea  mkoani Geita.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 22 Septemba 2023 na Meneja Masoko wa GST wakati akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa GST,  amesema kuwa  kitabu hicho ni toleo jipya ambalo limetoka mwaka 2023 likiwa na taarifa mbalimbali  zinazoonesha madini yanayopatikana nchini Tanzania kuanzia  ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Kijiji. 

Priscuss amefafanua kuwa toleo hili ni tofauti na toleo la zamani, hii ni kutokana na toleo hilo jipya kuwa na taarifa nyingi zaidi za uwepo wa madini(occurrences) na pia linaelezea  jiolojia ya mkoa husika pamoja na ramani yake.

Akizungumzia kuhusu  uwepo wa kitabu hicho ,Priscus ametumia fursa hiyo  kuwaalika wadau wote wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini  kutumia kitabu hicho  sambamba na taarifa nyingine za jiosayansi utafiti wa  jiosayansi ili kuongeza tija katika shughuli  za utafutaji na uchimbaji madini.

Sambamba na kitabu hicho GST  katika maonesho hayo imekuja na machapisho  mbalimbali ya jiosayansi  yanayoelezea jiolojia na aina mbalimbali za madini yanayopatikana nchini Tanzania.

Aidha , akielezea kuhusu uchunguzi wa madini maabara,  ametoa wito kwa wadau kutumia maabara ya madini ya GST kwani ni ya kisasa na majibu yake ni ya uhakika. Pia, amewaalika wadau wenye changamoto za kujua miamba au madini waliyonayo kufika katika banda hilo na  kupima bure ili watambue aina ya miamba na madini waliyonayo.

Maonesho ya Teknolojia ya madini kwa mwaka 2023 yanabebwa na kaulimbiu inayosema "Matumizi sahihi ya Teknolojia katika kuinua Wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger