Wednesday, 27 May 2020

TASAF KUANZA UTEKELEZAJI WA KIPINDI CHA PILI CHA AWAMU YAKE YA TATU NCHINI KOTE

...


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (aliyeketi katikati) akimsikiliza Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF , Zuhura Mdungi aliyesimama akitoa neno la kuwakaribisha Wandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye ofisi ndogo taasisi hiyo jijini Dar es salaam. Kulia kwa kwake ni Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge. 

***
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF umekamilisha mipango itakayowezesha kuanza kwa utekelezaji wa Kipindi cha Pili cha Awamu yake ya TATU kufuatia uzinduzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga amekutana na Wandishi wa Habari jijini Dar es salaam na kuwajulisha kuwa mipango ya kuanza utekelezaji wa kipindi cha pili ambayo imezingatia maelekezo ya Serikali inaelekea kukamilika.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema katika kutekeleza kipindi hicho cha pili, Mfuko huo utajikita zaidi katika kuhamasisha Walengwa kutumia zaidi huduma za kielektroniki hususani katika suala la ulipwaji wa ruzuku.

Aidha Mwamanga amesema mkazo mkubwa utawekwa katika kuhamasisha Walengwa kushiriki kwenye miradi ya maendeleo hususani katika sekta za elimu,afya maji na shughuli za miradi ya kiuchumi kwa kutumia utaratibu wa Ajira ya Muda na kisha kulipwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ametoa wito maalum kwa Walengwa wa Mfuko huo kuhakikisha kuwa wanapata huduma za simu ili waweze kunufaika na utaratibu mpya wa kulipwa kwa njia ya kielektroniki ambao umefanyiwa majaribio kwenye halmashauri za wilaya zipatazo 16 kwa mafanikio.

Bwana Mwamanga amezitaja halmashauri ambazo Walengwa wa TASAF hulipwa kwa njia ya kieleketroniki kuwa ni pamoja na Arusha, Ilala,Temeke, Kinondoni,Mpanda na Kigoma Manispaa. Nyingine ni Bagamoyo,Songea Manispaa,Kisarawe, Kilwa, Muheza ,Mkuranga, Bahi,Urambo, Siha na Unguja.

Mfuko wa Maendeleo yas Jamii-TASAF unatekeleza kipindi cha pili cha awamu ya tatu ambacho kilizinduliwa na Rais John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam ambacho kinatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi trilioni 2.032 ambazo zitatumika kutekeleza miradi inayolenga kuboresha huduma za miundombinu kwenye sekta za afya,elimu na maji na kutoa ruzuku kwa kaya zinazoishi katika mazingira duni sana ili ziweze kuboresha maisha.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger