MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akizungumza mara baada ya kukabidhi mashuka hayo katika anayemsikiliza ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akizungumza mara baada ya kukabidhi mashuka hayo katika anayesimamia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umekabidhi mashuka 50 kwa ajili ya vituo vya kutoka huduma ya Afya wilayani Pangani ikiwa ni kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora kwa wagonjwa wanapokwenda kupata matibabu kwenye maeneo hayo
Makabidhiano hayo yalifanywa na Meneja wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally katika halfa iliyoshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja Mwakababu alisema wamemkabidhi Mwenyekiti huyo kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Isaya Mbenje na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya afya wilayani Pangani wakiwa na dhamira ya bima ya afya ni kuhakikisha huduma zinakuwa bora.
Alisema ili pia lengo kubwa ni kuhakikisha wagonjwa wanapokwenda kupata huduma wakute mahali safi na salama ambayo yawawawezesha kupata matibabu kwenye mazingira mazuri yanayovutia.
“Kama mnavyojua NHIF tunajua Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ni mdau wetu mkubwa na Pangani ni eneo lake NHIF ikaona tumsapoti kwa upande wa afya kwamba anapopambana na maji kuhakikisha maji yanapatikana lakini pia kuhakikisha mazingira ya wananchi kwenye kupata huduma yaweze kuwa salama”Alisema Meneja huyo.
Hata hivyo alisema kwamba wataendelea kushirikiana na wadu wengine katika kuhakikisha huduma za bima ya afya zinaboreka huku akieleza kwamba wanataka wananchi wakifika kwenye maeneo ya kupata matibabu waweze kuona namna yalivyokuwa mazuri na safi wakati wote.
0 comments:
Post a Comment