Monday 25 May 2020

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye Atangazwa Mshindi wa Kiti cha Urais

...
Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho. 

Ndayishimiye ametangazwa kushinda baada ya kupata asilimia 68.72 ya kura zilizopigwa. 

Tume ya uchaguzi nchini Burundi ambayo imetangaza matokeo hayo moja kwa moja kupitia vyombo vya habari nchini humo, imesema Agathon Rwasa wa chama cha National Freedom Council (CNL) ambaye ndiye mshindani mkuu wa Ndayishimiye amepata asilimia 24.19 ya kura. 

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, asilimia 87.7 ya wapiga kura waliojiandikisha walishiriki uchaguzi huo. 




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger