Sunday 24 April 2022

WAZIRI GWAJIMA ATOA CHETI KWA SHIRIKA LA ICS KWA KUANZISHA MFUMO WA KUTOA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI BORA YA MTOTO KWA NJIA YA KIDIJITALI

...

Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima Ametoa Cheti cha Pongezi kwa Shirika la Wekeza kwa Mtoto na Kuimarisha Familia ICS la Mjini Shinyanga linalo tekeleza Miradi ya Kijamii katika Kupinga Ukatili wa Wanawake na Watoto Kupitia Utoaji wa Elimu ya Malezi na Makuzi Bora kwa Mtoto Baada ya kufanikiwa Kuanzisha Mfumo wa Elimu kwa Njia ya Mtandao kwa kutumia Simu Janja kwa lengo la kuhamasisha jamii itambue umuhimu wa Malezi Bora kwa Ustawi wa Watoto.

Soma pia: 

ICS YAJA NA MKAKATI WA KUTOA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI BORA YA MTOTO KWA NJIA YA KIDIJITALI


Aidha wengine waliopata vyeti vya Pongezi ni pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Ndugu Tedson Ngwale pamoja na Afisa Ustawi wa Mkoa huo Bi. Lyidia Kwesigabo kwa mshikamamo na uongozi mzuri wa wadau uliofanikisha kudhibiti Mauaji ya kinyama kwa Wazee kutokana na imani potofu za Kishirikina kuwa kila Mzee mwenye macho mekundu eti ni Mchawi.

Dkt.  Gwajima amesema Kuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi amaalumu ina mpango wa Kuanzisha Tuzo ya Siku ya Mashujaa wa Mapinduzi ya Kutokomeza Ukatili Kwa Wanawake, Watoto na Wazee ili Kuongeza Hamasa Kwa Jamii inayoshiriki Kupinga Vitendo Vya Ukatili wa Kijinsia hapa Nchini.


Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye Pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa Jamii inapaswa Kubadilika kuwa na Malezi bora kwa watoto ili kujenga Taifa lenye maadili mema

Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine amesema kuwa Shirika lina mpango wa kufikia watu laki sita (600,000) katika Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro na Simiyu kwa lengo la Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger