Monday 25 April 2022

AJALI YAUA WATU 8 KUJERUHI 19 NJOMBE

...



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah
**
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 8 na 19 kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Coaster T 287 CCY mali ya kanisa Katholiki Njombe iliyogongana na lori la makaa ya mawe.

Watu hao ni miongoni mwa Umoja wa vijana kanisa katoliki Jimbo la Njombe (UVIKANJO) ambao walikwenda kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila wilayani Njombe.

Orodha ya majina ya waliofariki kwenye ajali

Ajali ilitokea jana majira ya jioni katika eneo la Igima wilayani Wanging’ombe Barabara kuu (TANROADS) kuelekea mkoa wa Ruvuma.



Aidha amesema majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mji wa Njombe Kibena pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa huo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger