Sunday 24 February 2019

MAMA MBARONI KWA KUMCHOMA MTOTO ALIYEDOKOA CHAKULA

...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Eliza Denis (23) mkazi wa Makulu mkoani hapa kwa tuhuma za kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na kumchoma moto mikononi mtoto wake wa kambo, Jackson Denis (5) kwa madai ya kudokoa chakula.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi la Polisi linamshikilia mama huyo.

Kamanda Muroto alisema watu wamekuwa wakiendelea kujihusisha na matukio ya ukatili wa kijinsia, hususani kwa watoto hivyo Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“Huko maeneo ya Dodoma Makulu amekamatwa mama mmoja ajulikanae kwa jina la Eliza Denis ambaye ni mkulima na mkazi wa Dodoma Makuli kwa makosa ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na kumchoma mikononi mtoto wake wa kambo aitwae Jackson Denis mkazi wa Dodoma Makulu,” alisema Kamanda Muroto.

Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu shtaka hilo siku za hivi karibuni.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger