Friday, 31 July 2020

BOTI YAUA WATU 10 KUJERUHI 100 BAADA YA KUGONGA MWAMBA ZIWA TANGANYIKA

...

Ziwa Tanganyika

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, amesema kuwa watu 10 wamefariki dunia huku wengine 100 wakiokolewa, baada ya Boti iliyokuwa ikitokea maeneo ya Sibosa kupigwa na dhoruba kisha kugonga mwamba na kupasuka ndani ya Ziwa Tanganyika.

Kamanda Manyama ametoa taarifa hiyo hii leo Julai 31, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ambapo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Julai 30 majira ya saa 5:00 Asubuhi.

"Boti iloikuwa na watu karibia 100, na ilipokuwa ndani ya maji ilikumbwa na dhoruba kali na kugonga mwamba kisha kupasuka, na watu takribani 100 wameokolewa na kusababisha vifo vya watu 10, Wanawake3, Mwanaume 1 na watoto 6, zoezi la uokoaji linaendelea leo tuna mashaka huenda kuna miili ndani ya maji" amesema Kamanda Manyama.

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Uvinza Dkt Ruben Mwakilima, amesema kuwa miili imehifadhiwa katika Zahanati ya kalya na tayari miili ya watu wanne imekwishachukuliwa na ndugu zao.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger