Halmashauri ya wilaya ya misenyi imeendelea kutoa elimu kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuimarisha kamati simamizi za ulinzi na usalama zakata ili kuhakikisha zinakabiliana na matukio ya moto pamoja na uhalifu wilayani humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denice Mwila wakati akizungumza na Mpekuzi blog ofisini kwake ambapo ametaja mafanikio katika wilaya ya Misenyi kuwa ni pamoja na mbio za mwenge wa uhuru ambapo walikimbiza mwenge 27/4/2019 kimkoa walishika nafasi ya kwanza kikanda nafasi ya 2 na kitaifa nafasi ya 21.
Akizungumza Kanali Mwila Amesema katika sekta ya afya wanaishukuru serikali kuu kuwatengea shillingi million 400 ambapo fedha hizo zilitumika kujenga miundo mbinu mbalimbali katka kituo cha afya Bunazi ikiwa ni jengo la upasuaji,nyumba ya watumishi,jengo la kuhifadhi maiti,jengo la wagojwa wa nje (OPD) na njia ya kutembea kwa miguu.Na kuanzia mwezi wa nane upasuaji ulianza katika kituo cha afya Bunazi.
Pamoja na hayo amebainisha kuwa kampeni ya chanjo ya surua na polio ambapo ilifanyika kwa mafanikio wilayani humo kwa mafanikio makubwa na Chanjo ya surua Lubera walitegemea kuchanja watoto 35,581 na wameweza kuchanja watoto 37,774 sawa na 106% kwa upande wa polio walitegemea kuchanja watoto 17,286 waliochanjwa ni 16,594 sawa na 96%.
Kadhalika kwa upande wa mzingira katika mashindano ya usafi kitaifa wilaya ya misenyi ilishika nafasi ya 2 kati ya halmashauri 184 zilizoshindanishwa.
Pia kanali mwila amezitaja changamoto zinazoikabili wilaya hiyo kuwa ni pamoja na upungufu wa walimu 597 katika shule za msingi na walimu 72 kwa upande wa shule za sekondari na walimu wa masomo ya ya sayansi wapatao 19.
Vilevile ameitaja changamoto ya vyumba 10 vya madarasa nakusema kati ya vyumba hivyo vumba 8 tiyari vipo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji kadhalika kuna changamoto ya Viti na Meza kwaajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2020 .
0 comments:
Post a Comment