Sunday 29 December 2019

Rais Magufuli Arejesha fomu ya tamko kuhusu Rasirimali na Madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

...
Rais Magufuli amewasilisha fomu ya tamko kuhusu Rasirimali na Madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Dar es Salaam.

Fomu hizo zimewasilisha leo Jumapili Desemba 29, 2019 na katibu wake, Ngusa Samike kwa niaba ya Rais Magufuli aliyepo wilayani Chato mkoani Geita kwa mapumziko.

Akipokea fomu hizo, Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Harold Nsekela amempongeza Rais Magufuli kwa hatua hiyo akisema ametekeleza matakwa ya Kikatiba na Sheria ya Maadili.

“Viongozi kurejesha tamko ni jambo la kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 132 (5)b. Ibara hii inasema msingi wa maadili wa viongozi wa umma, itawataka watu fulani walioshika nafasi fulani za madaraka kutoa mara kwa mara maelezo kuhusu mapato, rasirimali na madeni yao.

“Katiba ndiyo inatatuka sisi viongozi kutoa maelezo haya kila mwaka. Ukija katika sheria yetu namba 13 ya mwaka 1995 kifungu 9 inaeleza kila mwisho wa mwaka kiongozi anatakiwa kumpelekea kamishna tamko la maandishi,” amesema Jaji Nsekela.

Jaji Nsekela amempongeza Rais Magufuli kwa kurejesha tamko la mapato, madeni na rasirimali zake kama kiongozi wa umma, huku akiwataka viongozi wasiorejesha kufanya hima kutekeleza mchakato huo kwa sababu zimebaki siku mbili pekee.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger