Saturday 28 December 2019

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU JIMBO LA SHINYANGA MJINI (PARIS YA TANZANIA) JIMBO LA MBUNGE MASELE

...
Mhe. Stephen Julius Masele


Jimbo la shinyanga mjini ama PARIS YA TANZANIA kama linavyojulikana na wenyeji wa mji huo ni moja ya mji wenye  maendeleo ya mwendokasi chini ya uongozi wa mbunge kijana wa jimbo hilo Mh Stephen Julius Masele maarufu kama PUTIN ambavyo wananchi wake wamembatiza kwa ukimya wake wenye kishindo wakimfananisha na Vladimir Putin Rais wa Urusi. Masele ambaye Pia ni Naibu Spika wa Bunge la Afrika( PAP). Tujikumbushe shinyanga ya kabla ya Masele na shinyanga ya sasa chini ya Masele:-


Shinyanga kabla ya Masele:-

1. Barabara ya lami moja tu kutokea stesheni ya treni kwenda kuelekea Japanese kona.

2.Maji ya visima yenye rangi kama chai ya maziwa. 
3. Hospitali moja tu ya mkoani hapakuwa na vituo vya afya na zahanati za kata.

4. Hapakuwa na shule ya SEKONDARI kidato Cha tano na sita na ufaulu ulikuwa chini sana. 

5. Umeme ulikuwa mjini kati tu. Mji ulikuwa hauna mvuto ukilinganisha na sasa. 


Shinyanga ya Masele(Paris ya Tanzania):-

1. Mitaa imepimwa na kupangwa, nyumba nzuri na makazi bora. 

2. Mtandao wa Barabara nzuri za lami zinazopitika na zenye taa za barabarani wakati wa usiku.Leo hadi ndala kuna lami....sikuwahi kufikiria lami itafika upongoji.

3. Maji ya zima Victoria vijiji na mitaa yote

4. UMEME mitaa na vijijini. 

5. Zahanati na vituo vya afya vyenye ubora wa huduma haswa kwa kina mama, wazee na watoto. Hospitali mpya ya rufaa Negezi,kituo Cha afya Cha kisasa Kambarage na kinajengwa kingine Ndembezi. 

6. Shule za kata zenye ubora Shycom iliyoboreshwa, Uhuru iliyoboreshwa, Mwasele, Old Shinyanga, Ibadakuli kwa uchache.

7.Kituo bora cha  kulea wazee wasiojiweza Kolandoto. 

8. Kituo bora cha watoto wenye mahitaji maalumu(Albinos) Ibinzamata. 

9. Makazi bora ya wananchi na nyumba za kisasa kwa wananchi na watumishi wa umma. 

10. Watu wazuri wenye afya, Kumbi bora za Starehe na viwanja vya burudani.

Hakika mwenye macho haambiwi tazama, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,Masele tumeona na tumeridhishwa na utendaji kazi wako.Hii ni kasi ya 5G ya maendeleo kutoka kwa mbunge kijana, msomi na mpenda maendeleo. Aluta kontinua Komredi Stephen Masele mbunge wa shinyanga mjini. Bado tunakuhitaji usikatishwe tamaa na wasaka tonge.

Ni Mimi Luhende Makwaia mkazi wa Shinyanga mjini
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger