Sunday 29 December 2019

Zao La Mpunga Na Mahindi Kuuzwa Kwa Mfumo Wa Stakabadhi Ghalani

...
SALVATORY NTANDU
Serikali nchini imeviagiza vyama vikuu vya ushirika kuhakikisha wanawauganisha wakulima wa zao la mahindi na Mpunga katika ushirika ili kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao hayo ili kuanzia mwakani 2020 yaanze kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Kauli hiyo imetolewa Disemba 28 mwaka huu na Naibu waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akizungumza na wakulima wa zao la tumbaku na pamba katika mkutano mkuu wa 24 wa chama cha Ushirika kahama (KACU) uliofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rai Dk John Pombe Magufuli imedhamiria kumkomboa mkulima kwa kuhakikisha ananufaika na zao analozalisha hivyo ni budi kuanza haraka mchakato wa kuwaunganisha wakulima wa mazao ya mahindi na Mpunga katika Ushirika.

“Haiwenzekani wakulima wetu  wa mpunga wananyonywa wa walanguzi wa mazao, gunia moja la mpunga wakati wa mavuno linauzwa elfu 35 na likiwekwa gahalani na wafanyabiasha mwezi disemba kama huu bei yake hupanda na kufikia shilingi laki mmoja na thelathini ndio maana tunataka waaingizwe kwenye ushirika”alisema Bashe.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi, Zainab Telack alisema zao la mpunga na mahindi liingizwa katika mfumo wa ushirika wakulima watanufaika kwa kuuza mazo yao kwa bei ya juu ilikinganishwa na sasa ambapo wanalazimika kuuza kwa bei zisizo rasmi.

“Halmashauri zetu zitaongeza mapato kutokana kodi za  uuzwaji wa mazao haya ambayo awali yalikuwa hayapewi kipaumbele kama vile tumbaku na Pamba zilizokuwa zinasimamiwa na vyama vya Ushirika”alisema Telack.

Telack pia aliwataka wakulima wa mpunga na mahindi kujikita na kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga mabwawa ya maji ili kuvuna maji ambayo yanapatikana kwa wingi katika msimu huu wa masika ambayo wataweza kuzalisha tena zao hilo kindi cha kiangazi na kupata faida mara mbili.

Nae Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) Emanuel Charahani alisema watahakikisha wanatekeleza agizo hilo ili wakulima wa mazao hayo waweze kupata faida kutokana na kilimo wanachozalisha ili kundokana na kuwanufaisha wafanyabiashara ambao wananunua mazo yao katika masoko ambayo sio rasmi.

sambamba na hilo Charahani amewataka viongozi wa vyama vyote vya ushirika nchini kuanzisha mfuko wa pembejeo ambao utakuwa na jukumu la kununua pembejeo zote za wakulima na  kuondokana na utegemezi wa kukopa fedha kwenye mabenki ambazo riba zake ni kubwa.

Paschal Robart na Rehema Shabani ni  miongoni mwa  wakulima wa zao la Tumbaku kutoka Halmashauri ya Ushetu walisema ushirika umesaidia wakulima wengi kupata faida kutokana na kuuza mazao yao kwa bei ya juu hivyo kujumuishwa kwa mazao ya mahindi na tumbaku kutaongeza vipato vya familia zao.

Mwisho.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger