
Afisa
wa polisi akisimamia mizigo ya abiria waliokuwa wakisafiri katika basi
la SB lenye namba za usajili T607 BDG lililokuwa njiani kuelekea Dar es
salaam kutoka Nachingwea na kupata ajali katika kijiji cha Mchinga
mkoani Lindi. Abiria 21 wamejeruhiwa na wamelazwa kwa matibabu katika
hospitali ya mkoa Lindi.
Basi
la SB lenye namba za usajili T607 BDG lililokuwa njiani kuelekea Dar es
salaam kutoka Nachingwea baada ya kupata ajali katika kijiji cha
Mchinga mkoani Lindi. Chanzo cha ajali hiyo bado kujulikana

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akiwafariji majeruhi wa ajali hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akimwangalia mmoja wa watoto ambao ni majeruhi wa ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment