Thursday 24 July 2014

ARUSHA:Mabweni ya Shule yateketea kwa Moto Monduli

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo asubuhi.
 
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ulizuka wakati wanafunzi hao wakiwa darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
 
Kikosi cha Zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo yameshateketea. Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu unafanywa kurejesha mabweni hayo katika hali ya kawaida.
 
TUPE MAONI YAKO KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger