Thursday 17 July 2014

AJALI YA NDEGE: NDEGE NYINGINE YA MALAYSIA YAUA ABIRIA 295 UKRAINE

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mwanajeshi mwasi akiwa karibu na eneo kulikoanguka ndege hiyo ya Malaysia.
Ndege ya shirika la Malaysian ikiwa na abiria 295 imeanguka
Mashariki mwa Ukraine ikiwa safarini kutoka Amsterdam hadi Kuala Lumpur kukiwa na madai kwamba ilidunguliwa.
Miili ya watu imetapakaa kila upande katika kile kinachoaminika kuwa masalia ya ndege hiyo ya muundo wa jet karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga,.
Ndege hiyo nambari MH17 ilikua inakaribia kuingia anga ya Urusi mawasiliano yalipokatizwa.
Rais wa Ukraine alielezea tukio hilo kuwa ni tendo la kigaidi huku waasi wakikanusha kuidungua. .
Inaaminiwa waasi hao wanaotaka kujitenga walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni.
Anga ya Ukraine haikufungwa rasmi lakini mashirika ya ndege ya Ujerumani, Lufthansa, Air France ya Ufaransa na Uturuki,yanaliepuka eneo la Ukraine Mashariki
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger