Monday 14 July 2014

WAZIRI GHASIA AFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NGAZI YA TAIFA MJINI MORO

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

picha ya pamoja
WAZIRI wa Tamisemi, Hawa Ghasia, Julai 14, mwaka huu, amefungua mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa  vilivyokuwa na usajili wa kudumu ngazi ya Taifa  kujadili maoni ya wadau mbalimbali ya kuboresha kanuni za uchanguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Oktoba 2014.
 
Mkutano huo pia unahudhuriwa na Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis na viongozi wengine wa Wizara hiyo.
 
Kwa mujibu wa Waziri wa Tamisemi, mkutano huo unawapa fursa viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya Taifa kupitia hoja na maoni ya wadau kama ilivyokwisha fanyika kwa makundi mengine.
 
Makundi  ambayo yameshatoa maoni na ushauri wao ni Asasi za Kiraia pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya nchini , maoni hayo na ushauri utakaotolewa na Viongozi hao ambayo Serikali itayafanyia kazi ili kupata kanuni bora za uchanguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014.
 
Katika mkutano huo wa siku mbili viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ngazi ya taifa wanashiriki akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba,pamoja na viongozi  wengine wa  vyama mbalimbali vikiwemo vya  Chadema, CCM, TLP na  NCCR MAGEUZI.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger