Thursday 24 July 2014

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (UDS,SUA,UDOM,SAUT ) WAKOSA IMANI NA SERIKALI YA TANZANIA,WALILIA PESA YAO YA FIELD,HII NI WIKI YA 5 HAWAJAPATA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
                                                            

Katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali hapa tanzania hadi mda huu hawajui hatima yao ni nini kwani tangu wasaini pesa yao ya field yapata   wiki 5 sasa.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanafunzi wa vyuo mbalimbali hapa tanzania wameonesha wazi kutokuwa na imani na uongozi uliopo juu kwani waliaihidiwa kuwa pesa haitachelewa tena.


Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha udsm kwa jina la john kozi ya engineering amesema kuwa hadi mda huu yupo field huku akiwa amekopa karibi ths 300000 kwa ajili ya kuendesha masomo yake awapo huko field.

Pia nilifanikiwa kufika SUA chuo cha kilimo kilichopo huko morogoro na kukuta vijana wakisubiria pesa yao ya field kwani hawajui hatma yao hadi leo.

Pia katika tembea zangu kufuatilia hilo suala nilifanikiwa kupitia shule moja iliyopo mkoano morogoro ijulikanayo kama mafiga secondary ambapo nilikuta walimu wengi wa practical wajulikanao kama field ambapo nilifanikiwa kukutana na mwalimu mmoja jina tumehifadhi ambae amesema kuwa hana imani na serikali ya tanzania.

Katika kufuatilia suala hili kwani mimi linanigusa moja kwa moja nlifanikiwa kupata namba ya simu ya Mfanyakazi bodi  ya mikopo dar es salaam ambae alisema kuwa pesa za wanafunzi hao zipo katika process hivyo wavute subra watazipata siku si nyingi kuanzia sasa,kwani hata wao hawapendezwi na kitendo cha kuchelewesha pesa za wanafunzi hao.

Taarifa hii ya imeandaliwa na mie innocent-the blogger ninaepatikana kwa simu namba +255768260834,kama una maoni,habari,au jambo lolote unalaotaka turirushe katika hii blog pendwa TANZANIA karibu sana,
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger