
WAKATI jana, Julai 9, 2014 George Otieno Okumu ‘Tyson ametimiza siku 40 tangu kifo chake kilichotokea kwa ajali mbaya ya gari mkoani Dodoma, mama mzazi wa marehemu, Gladys Okumu ameripotiwa kuugua ghafla nchini Kenya anakoishi.

“Kifupi tangu George (Tyson) amefariki dunia mama hayuko vizuri kiafya. Juzi (Jumapili) alizidiwa akakimbizwa Hospitali ya Aga Khan na kulazwa.
“Kikubwa ambacho naamini kimekuwa kikimsababishia tatizo hilo ni kitendo cha kutopewa undani wa ajali iliyomuua Tyson.

Naye ndugu mwingine wa marehemu Tyson aliye jijini Nairobi alipozungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu, alikiri mama huyo kusumbuliwa na presha na kulazwa.
Tyson alifariki dunia Mei 30, 2014 katika ajali mbaya ya gari aina ya Toyota Noah iliyotokea eneo la Gairo akitoka Dodoma mjini na wenzake watano ambao walinusurika kifo kwa kujeruhiwa na kutibiwa. Alizikwa Juni 14, mwaka huu kwenye Kijiji cha Siaya, Kisumu, Kenya.
0 comments:
Post a Comment