AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26), mkazi wa Sinza ya Kwaremmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za utafutaji maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.
Nilikimbizwa Hospitali ya Palestina kutibiwa na baada ya muda mguu ulionesha kupona kwa juu, lakini kumbe ndani kidonda kilikuwa kibichi na kiliendelea kulika bila mimi kujua.
“Mwanzoni mwa mwaka huu (2014) nikaanza kushangaa usaha mwingi unatoka sehemu mbalimbali ya mguu tena na harufu mbaya, mguu ukaonekana umeoza tena una matundu matatu, si unauona ulivyo, hata watu hawapendi kukaa jirani na mimi,” alisema Peter huku akionesha mguu wake huo.
“Ila namshukuru sana msamaria mwema anaitwa Louis, ndiye anayenisaidia kwa sasa,” alisema.
Aliongeza kuwa, baada ya kuhangaika kusaka nauli bila mafanikio, baadhi ya watu walimwambia atoe taarifa kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers ambayo yanasomwa na watu wengi Tanzania, atasaidiwa.
“Napenda kuwaomba Watanzania mnaosoma Magazeti Pendwa ya Shigongo mnichangie pesa ili nipate matibabu na nauli ya kurudi kwetu. Wenye kukuguswa na tatizo langu wanaweza kunisaidia kwa kutumia namba ya simu 0716 122 780, Louis.”
0 comments:
Post a Comment