MAPOKEZI
makubwa yanamsubiri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anayetarajiwa kuwasili
leo mchana mjini Mpanda kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani
Katavi inayoambatana na kutembelea, kukagua miradi kadhaa ya maendeleo
na kuhutubia mikutano ya hadhara.
Hii
itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa juu wa kitaifa kutembelea
mkoa wa Katavi tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani,
ziara ambayo itamfikisha pia katika mkoa jirani wa Rukwa.
Katibu
Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Katavi, Lauteli Kanoni amesema ziara ya
Waziri Mkuu mkoani humo itaanza leo na kutarajiwa kuhitimisha ziara yake
Agosti 23, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa ratiba, Waziri Mkuu atawasili leo mchana kwenye Uwanja wa
Ndege wa Mpanda kisha ataelekea Ikulu Ndogo ambako atasomewa taarifa ya
mkoa na kuzungumza na watumishi wa serikali katika viwanja vya ikulu
ndogo.
Siku
itakayofuata atakwenda katika Kijiji cha Majalila, kunakojengwa Ofisi
za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na kutembelea mradi wa maji kijijini
humo kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
Kwa
mujibu wa ratiba yake, anatarajiwa kuhutubia mikutano ya hadhara katika
kijiji cha Ndui kilichopo kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba na
katika uwanja wa Azimio, Manispaa ya Mpanda.
Aidha,
Agosti 22, mwaka huu Waziri Mkuu atafanya ziara ya siku moja katika
wilaya ya Mlele ambapo atawahutubia wananchi wa Inyonga katika
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kabla ya kuelekea katika Kijiji cha
Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe atakapokagua ujenzi wa daraja la mto
Kavuu na baadaye kuhutubia mkutano wa hadhara.
Waziri
Mkuu Majaliwa anatarajiwa kufanya majumuisho ya ziara yake Agosti 23,
mwaka huu katika ukumbi wa Idara ya Maji mjini Mpanda kabla ya kuelekea
wilayani Nkasi kuanza ziara ya siku tatu mkoani Rukwa.
0 comments:
Post a Comment