Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya amesema
utafunaji wa fedha za umma uliofanywa na watendaji ndiyo ulimtoa chozi
wakati akihojiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa
(Laac).
“Ni
kuwa kitu kilichonifanya (nitoke machozi) ni yale machungu ya
ubadhirifu wa wakuu wa idara na baadhi ya watendaji kufanya wizi kwa
kutumia carbon slip,” ameandika Mkandya kwenye ujumbe mfupi alioutuma
kwa mwandishi wa Mwananchi.
Katika
mahojiano mbele ya kamati hiyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa
mjini Dodoma mwanzoni mwa wiki, Mkandya aliulizwa swali na Mbunge wa
Viti Maalumu (CCM), Leah Komanya kuhusu ubadhirifu katika halmashauri
yake, na wakati akijieleza alikuwa akibubujikwa na machozi.
0 comments:
Post a Comment