Bodi ya Mikopo inapenda kuufahamisha Umma kuwa ‘database’ yake ya wanufaika wa mikopo ina taarifa zote muhimu zilizo sahihi.
1.0 UTANGULIZI
Kumekuwepo na taarifa zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, hasa gazeti la Jamboleo toleo namba 2541 la 23 Agosti, 2016 kuhusu Bodi ya Mikopo kuwadai wasionufaika na mikopo. Taarifa hizi zinalenga kuleta hofu na mkanganyiko usiokuwa wa lazima kwa wadau. Kufuatia hatua hiyo Bodi ya Mikopo inapenda kutoa ufafanuzi wa suala hili kama ifuatavyo:-

2.0 MADAI KUHUSU KUDAIWA MIKOPO KWA WALE WASIONUFAIKA
Bodi ya Mikopo inapenda kuufahamisha
Umma kuwa ‘database’ yake ya wanufaika wa mikopo ina taarifa zote muhimu
zilizo sahihi. Hii inatokana na utunzaji mzuri wa kumbukumbu za
ukopeshaji kuanzia hatua ya utoaji mikopo (loan allocation and
disbursement) hadi urejeshaji wake (loan repayment). Kutokana hamasa na
elimu inayotolewa, kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wanufaika wa mikopo
na waajiri wao kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo. Hivyo, katika
utekelezaji wa jukumu hilo, tumebaini kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa
baadhi ya wadaiwa kwamba ama hawakuwahi kukopa au hawajawahi kufikia
kiwango cha elimu ya juu.
Hadi sasa, imebainika kuwepo kwa baadhi
ya wanufaika ambao wanadai hawakujua iwapo fedha walizopatiwa na
serikali wakati huo zilikuwa za mkopo. Pia kuna wachache ambao vyeti
vyao vilitumiwa na ndugu zao kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu. Katika
hali hii, mdaiwa atalazimika kumtaja mtu halisi anayepaswa kukatwa deni
hilo ili Bodi iweze kusitisha makato hayo kwake.
Ili kupata ufumbuzi wa malalamiko hayo, Bodi inawataka walalamikaji kuzingatia yafuatayo:
2.1 Kwa mtu anayedai kwamba hajasoma
elimu ya juu kwa ufadhili wa serikali au Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu; mtu huyu awasilishe vielelezo vinavyodhihirisha kuwa
hakusomeshwa kwa ufadhili wa serikali.
2.2 Kwa mtu anayedai amekatwa mshahara
ingawa hajawahi kufikia kiwango cha elimu ya juu; mtu huyo anapaswa
kuwasilisha vielelezo vya kiwango cha elimu yake.
2.3 Iwapo kuna mnufaika wa mkopo anadai
amekatwa zaidi ya kiwango cha mkopo anaodaiwa; mnufaika huyo anapaswa
kuwasilisha vielelezo vinavyothibitisha kumaliza kurejesha deni lake.
Itakapothibitika kuwa kuna makato zaidi yalifanyika, basi kiasi
kilichozidi kitarejeshwa kwa mhusika.
3.0 HITIMISHO
Bodi inapenda kuwahakikishia wadau wake kuwa imetunza vizuri taarifa zote muhimu za wanufaika wa mikopo ambazo ndizo zinazotumika kwenye zoezi la urejeshaji wa mikopo. Kasoro ndogo ndogo zinazojitokeza zinatatuliwa kwa kufanya rejea kwenye kumbukumbu zilizopo.

Aidha, Bodi inaendelea kuwahimiza
wanufaika wote wa mikopo ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao
kuhakikisha wanawasilisha taaifa zao ofisi za Bodi au wanajaza taarifa
zao kweye fomu ‘Loan Inquiry Form’ iliyopo kwenye tovuti ya Bodi na
kuituma kwa anuani ya barua pepe info@heslb.go.tz ili kila mmoja ajulishwe deni lake na kuanza kurejesha.
Kwa mnufaika anayetaka kuanza kurejesha
mkopo wake baada ya kuwa amepata taarifa ya deni lake; aweke fedha
kwenye akaunti za Benki zifuatazo na kisha kuwasilisha hati ya malipo:
A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
0 comments:
Post a Comment