Wananchi
wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T
397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa
kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam
leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE
alijeruhiwa.
Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
Daladala hili likiwa limegonga gari namba T 458 CAN.
Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.
Na Dotto Mwaibale
MKAZI
wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo
alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB
linadodaiwa kuiba njia.
Ajali
hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo asubuhi
ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua
kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi.
Mkazi
wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu
kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.
"
Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala
lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande
ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari
dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro" alisema
Juma.
Alisema
baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili
likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.
Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.
Jitihada
za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo
hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa
simu mara kadhaa.
0 comments:
Post a Comment