Mr. Abdul Nondo, ni
mratibu wa mtandao wa wanafunzi TANZANIA (TSNP) mkoa wa kigoma. Kuna
program ameianzisha ya kuzungukia Shule mbali mbali TANZANIA,
Mr. Abdul Nondo
kuhamasisha wanafunzi kidato cha 1 hadi cha nne kutimiza wajibu wao, na
kuvaa majukumu Yao, na kujifungia Kwa Muda kutekeleza majukumu Yao, kuwa
na nidhamu, kujitambua nini wanapaswa kufanya,kuepuka makundi ambayo
hayana utaratibu wa kitaaluma,kupanga ratiba yao ya kujisomea,
changamoto wanafunzi wengi hawana utaratibu wa kujisomea, wazazi wao
mkoa wa kigoma hawana utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
Wanafunzi wengi wapo huru saana kufanya mambo ambayo si ya msingi Kwa
Muda huu wakiwa shuleni, ametembelea Shule ya RUBUGA na kirugu
sekondari kigoma, wanafunzi wamekiri hayo na wameahidi kubadilika
kuanzia leo hii,, hii Ndio kazi ambayo mtandao wa wanafunzi (TSNP),
tunayoifanya. Mtandao tumeunda TSNP CLUBS, ili tuendelee kupata taarifa
kutoka Shule hizo. Bado tunaendelea na kazi hiyo, baada ya kigoma ni
mikoa mingine.
Pia anapenda kushukuru afisa elimu sekondari manispaa ya kigoma ujiji, ndug,
Emmanuel L. Kitemi Kwa ushirikiano wake, pia napenda kumpongeza na
kumshukuru meya wa manispaa ya kigoma ujiji,ndug, hussein Ruvagwa, Kwa
sapoti yake kubwa na kutambua umuhimu wa elimu mkoa wa kigoma, mimi ni
Abdul Nondo mratibu wa mtandao wa wanafunzi TANZANIA (TSNP) mkoa wa
kigoma, na mjumbe wa idara ya haki na wajibu wa wanafunzi. No 0762
599672, page sauti ya wanafunzi Tanzania
0 comments:
Post a Comment