Tuesday, 23 August 2016

Waziri wa ulinzi atoa siku saba kwa halmashauri zisizochukuwa madawati JKT kuyachukua.

...
Waziri wa ulinzi nchini na jeshi la kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi ametoa siku saba kwa wabunge na halmashauri zao ambazo hazikuchukuwa madawati ya mgao wa awamu ya kwanza kutoka jeshi la kujenga taifa JKT kuchukuwa madwati hayo mapema huku akisisitiza kuwa atazishauri mamlaka za juu kugawa upya madawati hayo kwa majimbo mengine endapo halmashauri husika zitashindwa kutekeleza zoezi hilo.
Agizo hilo limetolewa mapema hii leo jiji Dar es Salaam jijini na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi amesema kati ya madawati 32387 ambao ni mgao wa awamu ya kwanza ni madawati 22,721 ambayo yamekwisha kuchukuliwa baada ya mradi huo kukamilika huku yakibaki madawati 9666 sawa na asilimia 30 ambayo hayajachukuliwa kitendo ambacho kinadaiwa kupelekea kukinzana na adhma ya kutatua changamoto ya madawati nchini.

Aidha waziri Mwinyi amesema matengenezo ya madawati awamu yapili yanaendelea vema na mpaka sasa madawati 20,000 yamesha kamilika ambapo ametumia nafasi hiyo kuyataka majimbo amabayo yapo katika mgao wa awamu ya pili kuanza kuyachukua.

Katika hatua nyingine mkuu wa jeshi la kujenga taifa JKT Brigedia Jeneral Michael Isamuhyo amekanusha uvumi uliokuwepo wa madawati yanayo gawiwa kutokuwa na ubora pamoja na kuharibika kabla ya kuwafikia walengwa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger