Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Nyakabungo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, anatuhumiwa kuwapa ujauzito wanafunzi watano wa shule hiyo.
Wanafunzi
hao wamebainika kuwa na ujauzito, baada ya uongozi wa shule hiyo kuona
mabadiliko kwenye miili yao na kuamua kuwapima afya.
Mkuu
wa shule, Boniphace Mjuli amesema baada ya kujiridhisha kuwa wana
ujauzito, waliwaandikia barua wazazi wao kuwaita shuleni kwa ajili ya
kuwaeleza matokeo ya vipimo na kuchukua hatua stahiki.
Wakizungumzia
tukio hilo, baadhi ya wazazi wa watoto waliokutwa na ujauzito wameiomba
Serikali ichukue hatua kwa wanaume wote wanaokatisha ndoto za wanafunzi
wa kike.
Mzazi
Yusuph Yusuph amesema ili kuwajengea mazingira mazuri wanafunzi wa
kike, lazima Serikali itekeleze sheria ya kuwakamata wanaume wenye tabia
za kutongoza wanafunzi na wahukumiwe kifungo cha maisha jela ili iwe
fundisho.
0 comments:
Post a Comment