Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeongeza nguvu kwa
kutuma askari wengine 80 katika oparesheni ya kusaka majambazi
inayoendelea katika maeneo ya Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha Polisi Dar
es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro,
amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana,
ikiwa na lengo la kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa
kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari
wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbade jiji Dar es
Salaam.
Amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine
wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya
waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni
hiyo bado inaendelea.
“Itakuwa ni kinyume cha utaratibu nikieleza kinachoendelea kwenye
operesheni, niwahakikishie silaha zilizochukuliwa
zinarudi,kinachoendelea nitawajulisha jumanne ili wananchi wajue kitu
gani kinaendelea,” amesema.
Ameongeza kuwa; “Mapambano ni ya kawaida sana, na ndio maana askari
polisi akifa kwa silaha ni jambo la kawaida sana. Operesheni tutaifanya
maeneo ya Vikindu, Pwani Dar es Salaam, sababu hii network (mtandao) ipo
na lazima tutaisafisha.Kama walidhani wataitawala DSM wamejidanyanya
lazima tutarudisha heshima ya jiji.”
Katika hatua nyingine, Sirro amesema amepata taarifa kuwa wapo baadhi ya
watu wanapewa fedha kwa ajili ya kufanya maandamano Septemba Mosi mwaka
huu ambapo ametoa onyo kwa watakaoshiriki kuwa watachukuliwa hatua kali
za kisheria kwa kuwa maandamano hayo hayajaruhusiwa.
“Wote tunajua madhara ya fujo, wazalendo naomba msishiriki, Wanaotaka
kujionesha wanapambana na polisi waje barabarani, ” amesema.
Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu
baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo,
na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa
kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.
Baadhi ya askari wakiwa tayari kwenye magari yao wakati wa kujiandaa kuelekea Vikindu kwenye mapambano
Vikosi hivyo vikitoka makao makuu ya kanda maalum ya Dar kuelekea kwenye mapamban
0 comments:
Post a Comment