Watu wasiojulikana
wamechoma ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Winning Spirit ya Arusha
na kufanya idadi ya shule zilichomwa moto ndani ya miezi miwili mkoani
hapa kufikia sita.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema jana kuwa tukio hilo
lililotokea saa saba usiku na taarifa za kiintelejensia zinaeleza kuwa
kuna kundi la watu linalofadhili watu wanaofanya uhalifu huo.
Alisema jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa kina kuubaini mtandao huo na kuchukua hatua za kisheria.
0 comments:
Post a Comment