Sunday 28 August 2016

CHADEMA: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

...
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kuhusu picha zinazoashiria shari.
Yanayowakuta Chama cha Chadema Tanganyika Ndio hayo hayo yanayo endelea kuwakuta Chama cha CUF na Wafuasi wao tokea miaka 20 ya Vyama Vingi ianzishwe Zanzibar. CCm wamekuwa wakitumia uniform za CUF kwakufanya shari na mauwaji, uharibifu wa Mali n.k.. Ili wapate Justification yakuwazuia Wazanzibari kudai haki zao.
Ndugu Watanzania kutoka Zanzibar na Tanganyika, lazima tuwe makini sana na kuwajuwa Maadui zetu nini lengo lao la ku.post Picha zinazoashiria SHARI, VITA kwakutumia Bendera na Uniform za Chama cha Democratic na Maendeleo (CHADEMA). Hii ni njia moja yakuonyesha kwamba Watawala hawa Haramu ( Vidiktetor Uchwara) wanajaribu Kutumia UV-CCM na Jeshi la Wananchi kufanya mazoezi ya SHAri ambayo yanaonyesha Watu/ mtu amevaa uniform akiwa na silaha za jadi. Lengo la picha hizi Ni kwamba Serikali haina Ushahidi wowote ule ambao wanawasingizia Vyama vya Upinzani kwamba ni Wachochezi. Sasa wanachokifanya nikujaribu Kujenga Twaasira yakuonyesha kwamba wanaofanya Mazoezi ya kivita ni Wanachama wa Chadema na wanataka kuhatarisha Amani ya Inchi ili Wa-JUSTIFY Kamata kama ya Wananchi wa vyama vya Upinzani vya Siasa na Viongozi wao. Kwataarifa zaidi hebu someni habari hii iliopo hapo chini:
Jioni hii zimeonekana picha za mtu ambaye anadhaniwa kuwa ni mwanamke ameshika silaha za jadi mikononi mwake, panga, upinde na mishale huku akiwa amevalia nguo zenye rangi na nembo za CHADEMA.
Mtu huyo ameonekana pia akifanya mazoezi huku nyuma yake kukiwa na bendera ya CHADEMA ambayo imeshikwa na watu ‘wanaoficha’ sura zao nyuma ya bendera hiyo.
Kwa mtazamo wa haraka picha hizo zinamuonesha mtu huyo akijiandaa kwa ‘shari’ ambayo bila shaka anaijua mwenyewe au na wenzake walioshirikiana naye kupiga hizo picha.
Tungependa kutaarifu umma kuwa picha hizo zisihusishwe kwa namna yoyote ile na Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1 kwa ajili ya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani kwa mujibu wa Sheria za Nchi, ambayo inatarajiwa kufanyika katika kutimiza wajibu na haki za kikatiba za Watanzania.
Tumeona ni vyema kuweka sawa jambo hili baada ya watu mbalimbali wapenda haki ambao wangependa kuona Operesheni UKUTA na Septemba 1, zikifanyika na kuendelea kwa amani ili kufikisha ujumbe mzito na muhimu unaokusudiwa kwa maslahi na matakwa ya Watanzania, kuanza kuhoji kuhusu picha hizo.
Lakini pia tumeamua kutozipuuzia picha hizo baada ya kuona dalili za maadui wa demokrasia na watetezi wa uvunjifu wa Katiba na Sheria za Nchi unaoendelea kufanywa na watawala kupitia kauli, matamko na vitendo, wakilenga kuzitumia picha hizo kuwatisha watu na bila shaka kujazia jazia vinyama kwenye vihoja vyao na propaganda nyepesi za kupindisha maudhui na madhumuni ya Septemba 1 na UKUTA kwa ujumla.
Chama kinalaani vikali matumizi ya nembo za chama yaliyofanywa na watu hao kwa namna inayoashiria shari na vurugu huku ikihusishwa na Operesheni UKUTA na Septemba 1. Waliozipiga na kuzisambaza mitandaoni wanajua makusudi yaliyowatuma kufanya hivyo na bila shaka watapaswa kuwajibika kwa walichofanya.
Tunapenda kusisitiza tena, kama ambavyo Chama kupitia kwa viongozi wakuu kimesema mara kadhaa sasa, Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1, vitatekelezwa kwa misingi inayothamini na kuzingatia uwajibikaji kwa maslahi mapana ya Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na kudai HAKI na KUPINGA UVUNJAJI WA KATIBA na SHERIA za Nchi kwa njia za AMANI.
Tumaini Makene
Mkuu wa Habari na Mawasiliano CHADEMA
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger