Muimbaji mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Bi. Shakila Said, atazikwa Jumamosi hii. Bi. Shakila alifariki ghafla jana Ijumaa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa shirikisho la muziki Tanzania,
Addo November, muimbaji huyo alifariki ghafla mara baada ya kumaliza
kuswali nyumbani kwake, Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa mwanae, Shani, mama yake alianguka na kupoteza maisha na
kwamba hakuwa akiumwa. Mazishi yake yanafanyika kwake Mbagala.
Bi
Shakila aliwahi kuwika na nyimbo kadhaa ukiwemo ule maarufu, MACHO
YANALIA MOYO UNACHEKA aliouimba akiwa na bendi ya JKT miaka ya 90.
Mwaka
1960, aliolewa akiwa na umri wa miaka 11 tu na kuachana akiwa na mtoto
mmoja kabla ya kuolewa tena na mwanaume aliyedumu naye kwa miaka 18 na
kuzaa naye watoto watano kabla ya mumewe kufariki mwaka 1975.
Alikuja
kuolewa tena na mwanaume mwingine aliyezaa naye watoto watano kabla ya
kuja kuolewa tena mara ya nne na mwanaume aliyezaa naye watoto wawili.
Alipokuwa
na mimba ya mtoto wake wa mwisho, Shani, mume wake alimwacha. Shani
alizaliwa mwaka 1993 na hapo ndipo alidai alichukia wanaume na kuamua
kuishi mwenyewe.
Pamoja
na kustaafu kazi JKT, Shakila aliendelea kufanya muziki na miaka miwili
iliyopita alikuwa akirekodi album yake Mama na Mwana ambayo ingekuwa na
nyimbo nane.
0 comments:
Post a Comment