Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba
kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla kuwa
lilifunga dirisha la maombi mnamo tarehe 15 Agosti 2016 ili kuruhusu
uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo. Uteuzi wa awamu ya
pili kwa waombaji wa cheti na diploma unatarajiwa kutangazwa tarehe 31
Agosti 2016.
Baraza
pia linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS)
utafunguliwa tena tarehe 1 Septemba 2016 hadi tarehe 15 Septemba 2016
ili kujaza nafasi za udahili zitakazokuwa wazi baada ya uchaguzi wa
awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale
ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu
waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuomba udahili hapo
awali.
Baraza
pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya
Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo bado unasubiri
mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa punde Baraza litakapopata
mwongozo kutoka Wizara yenye dhamana ya Elimu juu ya uchaguzi huo.
Waombaji wa vyuo hivi wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.
Aidha,
Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza waliofanya
maombi kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) wa Baraza kabla ya
tarehe 16 Julai 2016 ambapo Tume ya Vyuo Vikuu ilitoa tangazo juu ya
sifa za udahili na hawajafikisha sifa hizo kwamba unafanyika utaratibu
wa kuwarudishia fedha zao. Utaratibu huu utamalizika baada ya
kukamilisha tathmini ya idadi ya waombaji wa aina hiyo. Hivyo wahusika
wanaombwa kuwa na subira mpaka tathmimi itakapokamilika.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 26 Agosti, 2016
0 comments:
Post a Comment