Friday, 19 August 2016

Mahakama Yamwamuru Reginald Mengi Afike Kujieleza ni Kwa nini Asifungwe Gerezani Kwa Kupuuza Hukumu ya Mahakamagwe

...


MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi afike mahakamani kujieleza kwa nini asifungwe gerezani kwa kushindwa kutekeleza hukumu inayohusu malipo ya Sh bilioni 1.2.

Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu kujieleza kutokana na kushindwa kutekeleza hukumu iliyomtaka kuwalipa wafanyabiashara watatu, Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo,  Sh bilioni 1.2.

Alitakiwa kuwalipa fedha hizo kutokana na mgogoro wa malipo ya uuzwaji wa hisa katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani, Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu ili ajieleze kwa nini asifungwe gerezani kama mfungwa wa madai kama sehemu ya kukazia hukumu hiyo.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na wafanyabiashara hao kuwasilisha maombi katika hatua ya kukazia hukumu iliyotolewa Januari 28, mwaka huu na Jaji Agathon Nchimbi wa mahakama hiyo.

Katika hati ya kiapo ya wafanyabiashara hao, inadaiwa walifungua kesi dhidi ya Mengi na Kampuni ya K.M. Prospecting Limited, wakidai malipo yaliyokuwa yamebakia ya dola 428,750, 100,000 na 70,000, kwa kila mmoja.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger