WAZIRI wa Elimu, Sayansi naTeknolojia,
Profesa Joyce Ndalichako, ametoa mwezi mmoja kwa Mamlaka ya VETA kufanya
tathmini ya mafunzo wanayotoa katika vyuo vyote nchini ili kuona kama
yanaendana na matakwa ya serikali ya kuwa na wataalamu watakaofanya kazi
kwenye viwanda.
Aliagiza hivyo alipofanya ziara katika
chuo cha VETA kilichopo Kipawa, Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wa
ziara zake ambazo amekuwa akizifanya katika vyuo hivyo ili kuona namna
vinavyotekeleza majukumu.Alisema
katika vyuo ambavyo ametembelea amekuta changamoto za kuwepo kwa
mashine zilizoachwa bila ukarabati kiais cha kushika kutu na nyingine
nzima kutotumika wakati kukiwa na vyuo vinavyozihitaji.
“Ni vizuri kukawa na usawa wa mahitaji
katika vyuo vyote vya VETA kwenye kila mkoa, kulingana na uhitaji na si
vyuo vingine kuwa na vifaa na vingine kuvikosa”,alisema.
0 comments:
Post a Comment