Leo Jumamosi,Agosti 27,2016 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
limeendelea kufanya ya mazoezi ya utayari wa kukabiliana na vitendo vya
kihalifu.
Akiongoza mazoezi hayo,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro
Jumanne Muliro amesema mazoezi hayo aliyoyataja kwa jina la Kiingereza
““Route Match” ni ya kawaida kwa ajili ya kujiweka tayari kukabiliana na
uhalifu unaoweza kujitokeza.
Kamanda Muliro amesema wamekuwa wakifanya mazoezi mara kwa mara lakini
kilichofanyikani kubadilisha muda wa kufanya mazoezi na wataendelea
kufanya kila siku za Jumamosi.
“Huu ni mfumo huu ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria na kanuni
zinazolisimamia jeshi la polisi..tumefanya matembezi yanayohusiana na
ukakamavu,yanayojenga ujasiri kwa askari kumsaidia katika utekelezaji wa
majukumu yake,kwa hiyo kwa wananchi wanaoishi karibu na kambi ya jeshi
siyo wageni wa mambo haya ambayo huwa tunayafanya siku za Jumamosi
”,alieleza Muliro.
“Kilichofanyika leo tumepita mtaani asubuhi/mchana badala ya
usiku/alfajiri (saa 11 hadi saa 1.30) kama vile tumekuwa tukifanya
lakini lengo ni moja tu,watambue kuwa jeshi lao la polisi liko imara
katika kuwalinda raia na mali zao,kusimamia sheria za nchi na askari
mzuri ni yule mkakamavu,mwepesi ana uwezo wa kufikiri haraka kujua kile
anachokitekeleza kimesimamia sheria gani”,aliongeza Muliro.
Alisema mazoezi hayo ni ya kawaida na kusisitiza kuwa kwa wananchi ambao siyo wahalifu na walio wema wamefurahia mazoezi hayo.
Askari polisi wakiongozwa na kamanda Muliro walipita katika maeneo
mbalimbali mjini Shinyanga na maeneo huku wakiwa na vifaa mbalimbali vya
jeshi hilo ikiwemo magari,silaha na magari ya maji ya kuwasha.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo maeneo
mbalimbali walikopita askari polisi mjini Shinyanga,ametuletea picha
31…Shuhudia hapa chini
Hapa ni katika kambi ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga-Kulia ni
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
akitoa maelekezo kwa askari wa jeshi hilo kabla ya kuanza mazoezi mtaani
leo majira ya saa tatu asubuhi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akieleza kuhusu mazoezi ya "Route Match"
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo kabla ya kuanza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini kabla ya kuanza kufanya mazoezi mtaani
Askari polisi wakijiandaa kuanza kufanya mazoezi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
akifanya mazoezi na askari polisi wa jeshi hilo mjini Shinyanga
Askari polisi wakiendelea na mazoezi mtaani
Askari polisi wakiwa katika gari la maji ya kuwasha
Mazoezi yanaendelea katika eneo la Phatom mjini Shinyanga
Gari la maji ya kuwasha likiwa barabarani
Magari ya polisi yakiwa barabarani
Mazoezi yanaendelea
Askari polisi wakiwa ndani ya gari
Wananchi wakiendelea na shughuli zao huku askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Wananchi wakiendelea na safari zao
Askari polisi wakiendelea na mazoezi yao
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi mtaani
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
akizungumza kambini ambapo aliwaambia askari polisi kuwa watakuwa
wanafanya mazoezi ya namna hiyo kila siku za Jumamosi
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akisisitiza jambo
Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakiwa kambini baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Askari polisi wakiwa kambini
Askari polisi wakimsikiliza kamanda Muliro
Kamanda Muliro akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kufanya mazoezi
Waandishi wa habari wakiwa kambini
Askari polisi wakijiandaa kutawanyika baada ya kumaliza kufanya mazoezi.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment