Kwa muktadha huo, Wizara inawaagiza wachapishaji wote wa vitabu vya Darasa la Nne hadi Darasa la Saba ambavyo vina ithibati ya EMAC kuviwasilisha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kufanyiwa tathmini. Ili kufanikisha zoezi hili nakala nne (4) za kila chapisho ziwasilishwe kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania kabla ya tarehe 30 septemba, 2016. Baada ya muda huo kupita, vitabu vyote ambavyo havitakuwa vimewasilishwa na kuhakikiwa na Taasisi hiyo vitafutwa katika orodha ya vitabu vyenye ithibati.
Baada ya zoezi la uhakiki kukamilika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI, itafanya ufuatiliaji kwenye shule na maduka ya vitabu ili kuhakiki utekelezaji wa agizo hili.
Aidha, hatua stahiki zitachukuliwa kwa wauzaji/wachapishaji watakaoendelea kuuza vitabu vitakavyokuwa vimefutwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
0 comments:
Post a Comment