Mwanamme mzee zaidi duniani Sakari Momoi aaga dunia
Mwanamme mzee zaidi duniani raia wa Japan Sakari Momoi ameaga dunia mjini Tokyo akiwa na umri wa miaka 112.
Mwalimu
huyo mkuu wa zamani wa shule ya upili na baba wa watoto watano, aliaga
dunia kutoka na ugonjwa wa figo katika kituo kimoja cha kuwahudumia watu
wazee siku ya Jumapili.
Alikuwa ametambuliwa na Guinness World Records mwezi Agosti.
Momoi
alizaliwa mwaka 1903 mjini Fukushima na alikuwa mwalimu kabla ya
kupanda cheo na kuwa mwalimu mkuu kwenye shule kadha nyumbani kwao.
Alikuwa
na mazoea ya kusoma hasa mashairi ya Kijapan na pia alipenda kusafiri
sehemu mbali mbali nchini Japan na mkewe ambaye sasa pia marehemu.
Alitambuliwa na Guinness World Records mwezi Agosti.
Wakati
alipata cheti kutoka kwa Guinness World Records mwezi Agosti aliwaambia
waandishi wa habari alitaka kuishi miaka miwili zaidi. Guinness bado
haijatangaza mwanamamme mwenye umri mkubwa zaidi duniani baada ya Momoi.
Mwezi
Aprili mtu mzee zaidi na mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani
Misao Okawa kutoka Japan aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 117 na sasa
rekodi inashikiliwa na mmarekani Susannah Mushatt Jones ambaye ana umri
wa miaka 116.
Mtu
ambaye aliishi miaka mingi zaidi duniani kulingana na Guinness ni
Jeanne Calment kutoka ufaransa ambaye aliishi miaka 122 na siku 164 .
Aliaga dunia mwezi Agosti mwaka 1997.
0 comments:
Post a Comment