Saturday 11 July 2015

*MWENYEKITI WA CCM AFUNGUA KIKAO CHA KAMATI KUU, SASA NI MAPUMZIKO

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akifungua kikao cha Kamati Kuu leo asubuhi majira ya saa 5:45, kwa ajili ya kujadili jumla ya Ajenda Nne za Chama hicho.

Akizungumza wakati akifungua Kikao hicho Mwenyekiti alizitaja ajenda hizo kuwa ni pamoja na Kupitisha Irani ya Uchaguzi Mkuu wa 2015/2020, Kubatilisha kanuni iliyokuwa inaweka kikomo cha vipindi viwili kwa Madiwani na Wabunge wa Viti Maalum, Kupitisha Jina la Mgombea atakayepitishwa kugombea Urais wa Zanzibar na Kupitia na kupitisha Majina matano ya wagombea na hatimaye kupata majina matatu yanayokwenda katika mkutano Mkuu.

Kwa hivi sasa mkutano huo umesimama ambapo wajumbe wametoka nje ya ukumbi kwa ajili ya mapumziko. 
 Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano huo wakiwa ukumbini.
 Wajumbe wa Mkutano huo Wasira na mwenzake wakiteta jambo ukumbini humo.
 Mmoja wa wagombea aliyepita katika hatua ya Tano Bora, Benard Membe akiteta na wajumbe wa mkutano huo.
 Wengine ukumbini walikuwa na huzuni tu muda wote....
 Sehemu ya Wajumbe wa mkutano huo wakiwa ukumbini...
 Mjumbe akisoma kwa makini Document zake baada ya kupewa na kutafakari....
 Baadhi ya wajumbe wakisoma kwa pamoja Gazeti la mwananchi ukumbini humo.
 Baadhi ya Wazee wa Barala la maadili wakiwa ukumbini humo....
 Wanahabari wakisubiri kufunguliwa kwa mkutano huo.....
 Mjumbe Edward Lowassa, akitafakari.....
 Januari Makamba, aliyepita katika tano bora, akisalimiana na aliyekuwa mgombea mwenzake, Edward Lowassa.
 Waliopita katika tano bora Januari Makamba na Benard Membe wakikumbatiana kwa furaha ukumbini humo.
 AshaRose Migiro, aliyepita katika tano bora, akisalimiana na aliyekuwa mgombea mwenzake, Edward Lowassa.
Benard Membe, aliyepita katika tano bora, akisalimiana na aliyekuwa mgombea mwenzake, Edward Lowassa.
 Benard Membe akiteta jambo na mgombea mwenzake, AshaRose Migiro (kushoto) ni Samuel Sitta.
 Wagombea waliopita katika tano bora Migiro na Membe, wakipiga picha ya kumbukumbu na aliyekuwa mwenzao katika kinyang'anyiro hicho, Nyalandu (kulia),\.
 Benard Membe, akihojiwa na wanahabari wakati akiwasili kwenye viwanja vya Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo asubuhi.
  Januari Makamba, akihojiwa na wanahabari wakati akiwasili kwenye viwanja vya Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo asubuhi.
  Mjumbe, Raza, akihojiwa na wanahabari wakati akiwasili kwenye viwanja vya Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma leo asubuhi.
 Magari ya Polisi yakiwa doria katika eneo la CCM Makao Makuu..
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger