Wanawake hupenda sana kutumia marashi na vitu vingine kama sabuni zenye kemikali kwa ajili ya kujirembesha.
Baadhi yao wamekuwa wakipenda usafi wao
binafsi wakitumia vitu ambavyo baadhi yake ni hatari kwani wengine
wanapenda kusafisha sehemu zao za siri kwa kutumia sabuni zenye
kemikali, pafyumu yaani ‘deodorant’ au kupaka mafuta bila kujua madhara
yake.
Wanawake hao wanaotumia vitu hivyo wana
hatari ya kupata magonjwa ya zinaa au ya kuambukiza. Watafiti katika
Chuo Kikuu cha California, Marekani wanasema sabuni ngumu au hata za
maji, pafyumu ‘deodorant’ zinaharibu tishu muhimu zilizomo
ndani kabisa
ya uke.
Uharibifu huo wa tishu ndani ya sehemu
za siri humweka mhusika katika hatari ya kupata malengelenge, fangasi
vitu ambavyo huweza kusababisha kupata Ukimwi ikiwa watajamiiana na watu
wenye tatizo hilo.
Sabuni au dawa zinazouzwa na
wafanyabiashara zikitangaza kuboresha uke au kuondoa harufu kwenye
sehemu hizo nyeti nazo zina madhara.
Sabuni au mafuta yenye kemikali huchubua ngozi laini ya uke na ni rahisi vimelea vya magonjwa kuenea kwa urahisi.
Michubuko hiyo ambayo si rahisi kuonekana kwa macho ndicho chanzo cha kuingia kwa maradhi ya kuambukiza.
Kutokana na hayo ni wazi kwamba hakuna
haja ya kuweka kemikali, au pafyumu ukeni. Hizo sehemu zinahitaji
kuoshwa vizuri kwa maji safi.
Kemikali inapoingia ukeni inavuruga hali
ya kawaida na asidi inayolinda sehemu hizo ni vyema wanawake
wakaelimishwa kuhusu matumizi ya bidhaa zinaweka harufu nzuri katika
sehemu zao za siri, kurudisha bikira au mafuta ya kulainisha uke.
Wanawake wanaofanya usafi sehemu zao za
siri kwa kutumia bidhaa au baadhi ya vifaa visivyofaa kutumiwa ukeni
huweza kupata saratani ya shingo ya uzazi.
Bidhaa zenye kemikali ya ‘coal tar,’
ambazo mara nyingine huwekwa kwenye sabuni ama manukato na kutumiwa
ukeni na wanawake huweza kuchochea saratani hiyo.
Upo ushahidi wa kutosha kuwa kutumia
sabuni za kuogea za maji au ngumu katika sehemu za siri za ndani za
mwanamke kunaharibu uwiano wa bakteria na kusababisha bakteria
kuzalishwa kwa wingi na kumweka mwanamke katika hatari ya maradhi ya
zinaa ya kuambukiza.
USHAURI
Acha kutumia sabuni zenye kemikali au pafyumu sehemu za siri kwani husababisha hayo niliyoyataja hapo juu.
0 comments:
Post a Comment