Baada ya zoezi la uchukuaji na
urejeshaji wa fomu za kugombea ubunge kukamilika Majimbo yote yanatakiwa
kuanza zoezi la kura ya maoni tarehe 20-25 Julai mwaka huu kwa
kuzingatia Mwongozo wa Taratibu za Kura ya Maoni ambao umeshatumwa nchi
nzima.
“Kwa majimbo ya yaliyogawanywa
kila jimbo litafanya mchakato wake wa kura ya maoni kwa kusimamiwa na
mamlaka zilizotajwa katika mwongozo husika. Hii maana yake ni kwamba
zoezi la kura ya maoni litafanyika kwa siku 6 mfululizo. Kila kanda
inapaswa kuweka ratiba yake ya ndani katika muda huo na kuhakikisha kuwa
majimbo yote, ya zamani na mapya, katika kanda husika yakamilishe kura
za maoni ndani ya tarehe hizo.
“Kamati Kuu iliazimia pia kuwa
kura za maoni nafasi ya udiwani zitaanza kufanyika kuanzia tarehe 30
Julai hadi 5 Agosti, 2015. Hii maana yake ni kuwa zoezi la kura za maoni
kwa nafasi ya udiwani litaanza baada ya kumalizika kwa zoezi la kura za
maoni nafasi ya ubunge,” ameagiza Katibu Mkuu Dk. Slaa kupitia waraka
huo.
Aidha Katibu Mkuu amewaagiza
Waratibu wa Kanda za CHADEMA kusimamia utaratibu wa kuwatangazia
wananchi katika majimbo yote kwa njia anuai ikiwemo vyombo vya habari,
mitandao ya kijamii, matangazo kwenye mbao na nafasi mbalimbali za
hadhara ili Watanzania wote wapate fursa ya taarifa hiyo muhimu.
0 comments:
Post a Comment