Friday 10 July 2015

Makamu wa rais Maalim Seif ziarani Italia

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kuelekea nchini Italia kwa ziara ya siku nne ya kiserikali.

Katika ziara hiyo Maalim Seif anamuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Moh’d Gharib Bilal kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yanayofanyika mjini Milan nchini Italia.

Maonyesho hayo ya kimataifa yanazishirikisha zaidi ya nchi mia moja na arobaini (nchi 140), na yanatarajiwa kuhudhuriwa na wageni wapatao milioni 20 kutoka pembe zote za dunia.

Pamoja na mambo mengine, maonyesho hayo ambayo pia yanazishirikisha taasisi za kimataifa, yanabeba ujumbe wa umuhimu wa chakula chenye siha kwa afya bora za wananchi duniani kote, pamoja na kuzingatia matatizo ya upatikanaji wa chakula hicho duniani.

Kwenye ziara hiyo Maalim Seif anaambatana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na watendaji wengine wakiwemo Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi Mhe. Haji Mwadini Makame, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Zahra Ali Hamad na Mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe. Hamad Massoud Hamad.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger