Wednesday 22 July 2015

Mwenye nyumba amchukua mke wa mpangaji

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Ni siku nyingine tena tunakutana katika kona yetu ya Vituko Mtaani, leo tunapata simulizi kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbuyuni, Kata ya Azimio, Temeke jijini Dar es Salaam, Selemani Mponyo (pichani), hapa anaanza kusimulia kisa cha kusisimua.
“Mambo mengine ni aibu kuyaongea kwa umri kama wetu lakini ngoja nisimulie ili watu wajifunze. Ni kipindi kirefu sasa tangu niamue kesi iliyonishangaza sana.
“Siku moja walikuja mke na mume ofisini, mume akimtuhumu mkewe kwa kutembea na mwenye nyumba
wao. Alidai kuwa mkewe ndiye aliyetafuta chumba na baada ya kupata, akamtaka yeye kwenda kulipia, lakini alifanya hivyo bila kujua kuwa tayari mwenye nyumba alishampa maneno matamu mkewe.
“Alisema muda mfupi baada ya kuhamia katika makazi hayo mapya, alianza kuingiwa na wasiwasi baada ya kuona ukaribu kati ya mkewe na mwenye nyumba unavuka mipaka, maana yule jamaa alikuwa akimletea zawadi mara kwa mara na kuwasiliana kwa meseji za mapenzi usiku.
“Mume alidai baada ya uchunguzi wake, akathibitisha kuwa mkewe anashiriki mapenzi na mwenye nyumba, akampa kibano kikali akakiri jambo hilo na akaomba msamaha akidai hatarudia. Mume pia akaenda kwa mwenye nyumba ambako jamaa naye alikiri kitendo hicho, lakini akadai mkewe ni mwenye tamaa kwani alimtaka awe anampa hela ya kodi inayotolewa na mumewe.
“Mwanaume huyo alidai baada ya mwenye nyumba kukubali aliamua kumfukuza mkewe lakini watu walimshauri si busara ndiyo maana akaamua kuja kwangu nipate kumshauri.
“Kesi hii ilinishangaza sana, nilimshauri kama kweli ameamua kumsamehe ni vyema akahama ule mtaa na wasahau yote yaliyopita.”
Kama una kituko cha kusisimua wasiliana nami kupitia namba ya simu iliyopo hapo juu, angalizo ni lazima awe mjumbe wa mtaa, mwenyekiti au afisa mtendaji.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger