Wednesday 22 July 2015

Ray c awapiga mizinga wanaomchumbia

...
IMG_0380


MAKUBWA! Mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C,’ amedaiwa kuwageuza mtaji wanaume wanaojitokeza kumchumbia kwa kuwapiga mizinga ili ajipatie ‘chochote’ (fedha), Risasi Mchanganyiko lina ‘full’ stori.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanaume aliyejitambulisha kwa jina la Aboubakar ambaye alifunga safari mpaka kwa Ray C kwa lengo la kutaka kumuoa wiki chache baada ya mwanadada huyo kutangaza kutafuta mume mwenye vigezo alivyovitaka, baada ya kuchati na kumueleza kuwa anataka kumuoa, alishangaa kuona mwanadada huyo anampiga mzinga.
Kijana  Abubakar Ally ‘Babuu’.
Aboubakar alisema Ray C alimuomba amtumie shilingi laki moja kwa njia ya simu ambapo jamaa huyo alikataa na kutaka wakutane kwanza ndiyo wapeane kiasi hicho cha fedha. Msanii huyo alimtaka jamaa wakutane Mbezi-Garden lakini amtumie kwanza pesa hizo.
Akizidi kumwaga ubuyu, Aboubakar alisema alianza kumuona Ray C kama mtu wa mizinga kwa kung’ang’ania atumiwe pesa hiyo wakati hawajakutana na kuongeza kuwa alimpigia simu ili kupata uhakika zaidi kama kweli akimtumia pesa hiyo watakutana kwenye hoteli hiyo, lakini alimhakikisha kuwa endapo atamtumia watakutana.
“Unajua nini, ningeweza kumtumia kama tungekutana ana kwa ana lakini ndiyo kwanza nimewasiliana naye ananipiga kirungu kikubwa hivyo je, nikiwa naye si nitakuwa natoa mamilioni, kama ndiyo hivyo amenishinda,” alisema Aboubakar.
IMG_0375….Akigonga geti nyumbani kwa Ray C.
…Kama hiyo haitoshi, mwanaume mwingine kutoka Mwanza aliyeongea na mwandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini, alidai kuwa Ray C alimwambia amtumie shilingi elfu 40 kwa ajili ya mafuta kwenye gari lake kabla hata hajakutana naye jambo lililomfanya aachane naye.
“Aliniambia nimtumie shilingi elfu 40, sasa nikaona mtu mwenyewe ndiyo kwanza ninaongea naye, anaonekana anapenda hela sana huyu mdada na mimi nimekata tamaa,” alisema mwanaume huyo.
Mwandishi wetu alimtafuta Ray C na kumsomea mashtaka yake ambapo alisema wanaume wengi wamekuwa wakimsumbua baada ya kutangaza kutaka mume na kudai kuwa wanaume hao ni washamba hivyo ameamua awaombe hela ili wasimpigie tena.
“Wapuuzi sana hao, sasa kuwakatiza nawaambia tuma milioni baada ya hapo hawanisumbui tena,” alisema Ray C na alipoulizwa kama haoni anajikosesha bahati ya mume mwema kwa kuwaomba hela, alisema wanaume wengi wanaopiga ni washamba tu kwa kuwa yeye hataki kulea mwanaume bali anataka kulelewa
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger