Saturday 11 July 2015

LULU MAHABA UPYAA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mwandishi wetu BAADA ya kujituliza kwa muda mrefu, staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametengeneza kichwa cha habari upya
baada ya picha zinazomuonesha akiwa kimahaba na mchekeshaji maarufu nchini, Stan Bakora kunaswa, Risasi Jumamosi lina mchapo kamili.

Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na Stan Bakora.
Tangu apate msala wa kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba na kuachiwa kwa dhamana mwaka 2013, Lulu ‘alikauka’ kwenye vyombo vya habari hususan kwa kuandikwa na habari zinazomhusisha na wanaume. 
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Lulu na Stan Bakora wamekuwa kwenye mahaba motomoto jambo ambalo limekuwa likiwashangaza wengi maana imekuwa ghafla na hakuna aliyewahi kutegemea kama wawili hao wanaweza kuwa karibu.

“Ishu iko hivi, Stan na Lulu kwa sasa ndiyo habari ya mjini. Wana ukaribu wa hali ya juu. Wanaitana baby, mara honey wakati mwingine my love. Kama hamuamini fuatilieni wenyewe mtathibitisha,” kilieleza chanzo chetu.
Lulu akimbusu Stan Bakora shavuni.
CHANZO KINGINE
Mara baada ya ubuyu huo kutua kwenye dawati la  Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alianza kuichimba habari hiyo na kufanikiwa kunasa picha tofauti za Lulu akiwa kimahaba na Stan Bakora.“Mimi nina picha za Stan na Lulu wakiwa kimahaba. Kama vipi ngoja niwatumie. Tena kuna moja ilitupiwa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua gumzo,” kilieleza chanzo hicho na kumtumia picha hizo mwanahabari wetu.

Staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
WALIPIGA KWENYE FUTARI YA WEMA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, picha hizo ambazo mojawapo inamuonesha Lulu akimbusu Stan, walizipiga juzikati walipoalikwa kwenye futari na mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’.“Hizi picha walipiga kwenye mwaliko wa futari ya Wema kule Mbezi  (Dar) katika Hoteli ya Ramada ambapo kwa macho yangu niliwashuhudia wakipeana kampani ya kimalovee.
AMBEBEA POCHI
“Kama hiyo haitoshi, kuna wakati Stan alionekana akiwa amembebea Lulu pochi yake. Yaani ni full kupeana kampani hadi raha.

LULU AITWA SHEMEJI
“Watu walikwenda mbali zaidi kimawazo baada ya kusikia Kitale akimuita Lulu shemeji kutokana na uhusiano wake na Stan,” kilisema chanzo hicho.

USHAHIDI WA SMS
Wakati mwanahabari wetu akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa SMS zilizokuwa zinatoka kwenye simu ya Stan kwenda kwa Kitale wakipeana ushauri wa uhusiano huo mpya ambapo Kitale alionekana kumshauri Stan amuoe Lulu.

Stan Bakora: Vipi kuhusu Lulu?
Kitale: Oa babu. Ila kuna kijana anamnyemelea, anaitwa Mirror.

STAN AFUNGUKA
Mwanahabari wetu baada ya kupata maelezo hayo, alimpigia simu Stan ili aweze kuzungumzia uhusiano wake na Lulu ambapo alidai ni mtu wake wa karibu.


“Huyu ni baby wangu tu, ingawa sitahitaji sana kuweka wazi mambo mengine yaliyojificha kati yangu na yeye maana najua kuna watu wengi wanatamani kutusambazia mambo ambayo si mazuri kutokana na ukaribu wetu, ila ningependa kwako wewe utambue kwamba Lulu ni mtu wangu sana na tumekuwa tukiitana majina yoyote kwa kuwa hakuna dosari ya aina yoyote baina yetu,” alisema Stan.
LULU ANASEMAJE?
Jitihada za kumpata Lulu ili aweze kuzungumzia uhusiano wake na Stan  hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kutokuwa hewani hadi tunakwenda mitamboni. Jitihada zinaendelea.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger