Saturday 11 July 2015

5 BORA CCM, DOM KIMENUKA!

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
5 BORA CCM, DOM KIMENUKA! WAKATI wa mchakato wa kuipata orodha ya tano bora ya
wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma, mtafaruku wa aina yake umeibuka miongoni mwa wapambe wa wagombea waliokuwa na hofu ya kukatwa majina yao, Risasi Jumamosi limeelezwa.


Wajumbe wa kamati kuu ya CCM.
Kikizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu juzi jioni, chanzo kilichopo Dodoma kilisema baadhi ya wapambe wa wagombea hao, wameibua mtafaruku kwani hawakufurahishwa na mchakato wa mchujo huo kwani wamenusa majina yanayopenya kabla, kitu ambacho siyo sahihi.
“Huku ni vurugu tupu hakuna anayeamini kama huu mchujo unakwenda kwa haki watu wanarushiana madongo mwanzo mwisho, wanatishiana hadharani,” kilieleza chanzo chetu.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni juzi, bado majina ya tano bora ya wagombea urais yalikuwa hayajapatikana ambapo yalitarajiwa kutangazwa jana Ijumaa.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger