Mshambulizi
wa Uruguay na Liverpool ya Uingereza Luiz Suarez sasa amemuomba msamaha
mlinzi wa Italia Giorgio Chellinii kufuatia tukio la kumng'ata timu
hizo zilipokuwa zicheza mechi ya mwisho ya makundi huko Brazil.
Suarez
aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ''baada ya kuketi
nyumbani na familia yangu na kutulia imenijia kuwa tukio la kumng'ata
Chellini ni la kusikitisha na kwamba sitarudia tena .
Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa dunia 1-0 jumanne iliyopita.“ninajutia
sana tukio hilo na ninamuomba msamaha Chellini .ukweli ni kwamba
anauguza jereha la kuumwa baada ya kugongana naye katika mechi hiyo .''
0 comments:
Post a Comment