
SAKATA la wafanyakazi wa
ndani kunyanyaswa na mabosi wao limeingia katika sura ya kipekee, safari
hii mabosi wamegeukwa ambapo mmoja amedaiwa kuuawa na hausigeli wake
aliyetajwa kwa jina la Valentina Karenge (17).
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyakazi huyo wa ndani mkoani Singida kudaiwa kumuuua tajiri yake kwa kumchoma kisu sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyaswa naye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP) Geoffrey Kamwela alisema tukio hilo la aina yake lilijiri saa 10 alfajiri Juni 29, mwaka huu eneo la Sabasaba, Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida.
Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Pendo Justine Kiula (24) ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.
Alisema baada ya polisi kuendesha msako kwa kushirikiana na raia wema hatimaye walifanikiwa kumkamata msichana huyo majira ya saa 8 mchana uliofuata maeneo ya Uwanja wa Ndege akiwa katika harakati za kutoroka.
Alisema ilipofika saa kumi kasoro usiku, alishituka kugongewa mlango na marehemu na alichokisikia akikizungumza ni; Kwa jina la Yesu nakufa, kwa jina la Yesu nakufa.’

“Nilipotoka chumbani, nilimkuta ameanguka chini huku akiwa ameshikilia pale alipochomwa kisu huku damu zikiendelea kumtoka.” Alisema mpangaji huyo.

Marehemu alizikwa Julai 2, mkoani Singida. Ameacha mtoto mmoja.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake. Amina.
0 comments:
Post a Comment